
MIRUNGI ni aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unevunyevu na milima yenye urefu wa kati ya futi 4000 hadi 9000.
Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika mikoa ya Arusha, Kilimajaro, Manyara na Tanga.
Hata hivyo kiasi kikubwa cha mirungi itumikayo nchini huingizwa isivyo halali kutoka nchini Kenya.
Mirungu hujulikana kwa majina mengi kama vile Miraa, Mbaga, Mogoka, Veve, Bomba na Kashamba.
Kwa mujibu wa wakala wa Maabara ya mkemia Mkuu wa Seriali ya Tanzania, Mirungi ina kemikali inayojulikana kama “Cathinone”, ambayo mtumiaji akitumia hukosa hamu ya kula.
Madhara mengine kwa mtumiji wa Mirungi ni kutokwa na vidonda vya mdomoni na tumboni, kukosa choo, kupungukiwa maji mwilini, kupata shinikizo la damu, kupungukiwa nguvu za kiume, mwili kuwasha, kupata maumivu makali ya kichwa na kuharibika ini.
Sheria ya dawa za kulevya ya mwaka 1995, inasema kuwa, ni kosa la jinai, kutumia, kuhamasisha matumizi, kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na mirungi.
No comments:
Post a Comment