Tuesday, July 14, 2015
CHAMA CHA MAPINDUZI NA HISTORIA YAKE.
Chama cha Mapnduzi CCM kinaendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya chuki na msambaratiko wa umoja wa
kitaifa, amani na mshikamano. Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania. CCM ilizaliwa 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume. Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment