Saturday, August 15, 2015

Yafahamu Madhara ya Ulaji wa Chumvi kupita kiasi Mwilini

CHUMVI ni dawa ya mboga.” Watu wengi hupenda kusema hivyo. Tangu enzi na enzi, chumvi ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula. Mbali na kuwa na madhara inapotumiwa vibaya, lakini bado ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Chumvi ni aina ya madini yenye umuhimu na faida nyingi kwa mtumiaji akama atatumiwa kwa kiasi kinachotakiwa kitaalamu kwenye mlo wake. Kimsingi, chumvi si rahisi kuikosa kwenye nyumba zetu. Hupatikana kirahisi kwa kuwa bei yake ni nafuu, ikikilinganishwa na viungo vingine vya jikoni. Wataalamu na wanasayansi wanasema kwamba matumizi ya chumvi kupita kiasi, ni kichocheo cha magonjwa ya moyo, yanayochangia vifo vingi vya watu duniani kwa sasa. Ingawa watu wengi wanaichukulia chumvi kama kiungo cha kawaida tu kisichokuwa na umuhimu mkubwa, lakini inapaswa kufahamika kuwa kiungo hicho kina umuhimu mkubwa katika afya ya mwanadamu. Ukweli ni kwamba chumvi ni madini yanayosaidia kuhifadhi maji mwilini, kudhibiti kiwango cha sukari mwilini, kusaidia tezi ambazo kitaalamu zinaitwa Thyroid, na zaidi husaidia katika suala zima la upatikanaji wa usingizi. Wataalamu wa afya wanashauri utumiaji mzuri wa chumvi katika vyakula, kwa kuwa inapotumika vibaya, huwa inasababisha madhara mbalimbali kwenye mwili wa mwanadamu. Utafiti uliofanyika Machi, 2013, kabla ya kuwasilishwa katika mkutano wa Chama cha Wenye Matatizo ya Moyo mjini, New OrleĆ”ns, Marekani, ulibainisha kuwa matumizi ya chumvi kupita kiasi kulichangia vifo vilivyohusiana na matatizo ya moyo kiasi cha takriban watu milioni 2.3 duniani kote. Kwa mujibu wa Radio Tehran ya Iran, asilimia 42 ya watu hao walikufa kutokana na magonjwa ya moyo, wakati asilimia 41 walifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kiharusi. Hii ni kwa mujibu wa vifo vilivyorekodiwa mwaka 2010 pekee. Idadi hii inajumuisha walaji wa chumvi nyingi iliyomo kwenye vyakula vingi vya makopo na maboksi, ambavyo hutumia chumvi zenye kiwango kingi cha Sodium inayoongezwa wakati wa kutengenezwa kwa vyakula hivyo viwandani. Katika utafiti huo, iligundulika kuwa nchi inayoongoza kwa watu wake kula chumvi nyingi kuliko nchi zote duniani, ni Kazakhstan iliyoko Asia ya Kati, jirani na nchi ya Urusi. Kwa mujibu wa utafiti huo, kwa wastani Wakazakhstan hula kiasi cha miligramu 6,000 za chumvi ambayo ni zaidi ya vijiko vidogo vitatu kila siku moja. Katika ripoti ya utafiti huo, nchi za Kenya na Malawi ndizo zenye kiwango kidogo zaidi cha matumizi ya chumvi duniani, kwa wastani wa miligramu 2,000. Wastani wa kiwango cha chumvi kinachokubalika kiafya, ambao mtu anatakiwa kula kwa siku ni miligram 2,300 tu. Hii ni sawa na kijiko kidogo cha chumvi kwa siku nzima. Inapozidi kiwango hicho mwilini, chumvi hiyo husababisha matatizo mengine ya kiafya. Lazima tuzingatie hili. Wataalamu wa afya wamekaririwa wakisema kwa watu wale wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu, wanatakiwa kutozidisha kiasi cha miligramu 1,500 kwa siku. Wapo wanaopinga kipimo hiki wakidai kwamba watu wanaochuruzikwa na jasho kupita kiasi, wanaofanya kazi za sulubu, wanamichezo na wanaoishi katika nchi za joto, wanatakiwa kula chumvi zaidi. Hata hivyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Phili Chilo, anasema: “Chumvi ikitumiwa vibaya husababisha maradhi ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo. “Baadhi ya magonjwa hayo ni pamoja na moyo kushindwa kusukuma damu, kutanuka na mengineyo yanayoweza kusababisha mtu apatwe na mshituko wa ghafla wa moyo na kupoteza maisha.” Hali hiyo inachangiwa pia na matumizi yasiyo sahihi ya chumvi. Ili kuepuka maradhi hayo, jamii inashauriwa kuwa na tabia ya kupima afya. Kwa hiyo, ni vema kutumia kiwango kinachohitajika cha chumvi wakati wa kupika chakula kwa kuwa chumvi mbichi ya kuongezea mezani, si nzuri kiafya, inapaswa kuepukwa. Wananchi wanashauriwa pia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya chumvi kwenye vyakula. Aidha, kwa wale wanaopenda kula vyakula vya makopo na vifungashio vingine, wanashauriwa kusoma maelekezo ili kufahamu kiasi cha chumvi iliyomo kwenye vyakula hivyo. Madhara ya chumvi mwilini Kuna matatizo makubwa mawili kwenye ulaji wa chumvi ambayo hufanya chumvi kuwa hatari. Mosi, ni watu kuzidisha kiwango cha chumvi kwa kuweka chumvi nyingi kwenye vyakula vyao au kununua vyakula vilivyokwisha kutengenezwa na kuwekwa chumvi nyingi. Pili, kula chumvi isiyo sahihi, kwa maana ya chumvi inayopatikana kiasili na si kwa kutengenezwa. Ili kupata faida ya chumvi iliyokusudiwa, ni lazima siku zote tutumie ile ambayo haijatengenezwa na kuongezewa kemikali nyingine zenye madhara kwa mwili. Chumvi asilia huwa na virutubisho muhimu ambavyo madini ya Sodium na Chloride, ambavyo huingia mwilini kwa kula lishe sahihi. Kwa bahati mbaya sana, chumvi inayotumiwa na watu wengi haina madini hayo ya kutosha, kutokana na kutengenezwa upya viwandani kwa kusafishwa (Refined). Kwa mujibu wa maelezo ya Taasisi ya Maradhi ya Shinikizo la Moyo ya Uingereza, chumvi ikizidi mwilini husababisha maradhi ya moyo, saratani ya tumbo, matatizo ya figo, ubongo kuwa msahaulifu uzeeni, maradhi ya mifupa, pumu na kadhalika. Madhara mengine kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ni kwamba kutodhibiti ulaji wa chumvi, huchangia ongezeko la vifo na maradhi kama vile kiharusi, figo kushindwa kufanya kazi, mshituko wa moyo, na macho kupoteza uwezo wa kuona na kadhalika. Faida ya chumvi mwilini Utumiaji sahihi wa chumvi na kwa kiwango kinachotakiwa, una faida nyingi mwilini. Faida hizo ni pamoja na kuimarisha na kudhibiti shinikizo la damu, kuboresha ufanisi wa misuli ya mwili, kuboresha ufanisi wa ubongo na kadhalika. “Chumvi ikitumiwa kwa kiasi kinachotakiwa, haina madhara mwilini. Chumvi ikitumiwa vizuri, ni dawa mwilini. Lakini ikitumiwa vibaya, huleta madhara makubwa ya kiafya kwa walaji pasipo wao kufahamu,” anasema mmoja wa wataalam wa mambo ya vyakula na kuongeza. “Lakini, ili kupata faida hizo, ni lazima chumvi yenyewe iwe ni ya asilia ambayo haijachakachuliwa wala kuongezwa kemikali nyinginezo. Kwa maana nyingine, ulaji wa chumvi iliyoondolewa madini yake muhimu na kuongezwa kemikali nyingine pamoja na kula kupita kiwango cha kawaida, husababisha chumvi kuwa na madhara badala ya faida mwilini, hivyo kugeuka na kuwa chanzo cha matatizo ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo. Kwa hali hiyo, kila mtu hana budi kupunguza matumizi ya chumvi, kutumia chumvi asilia muda wote, kwa maana ya chumvi inayochimbwa na kuuzwa kienyeji ambayo ni bora zaidi kuliko ile inayopitia viwandani ambapo huondolewa Sodium na Chloride, na wakati mwingine huongezwa kemikali nyingine hatari zaidi. Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema ulaji mkubwa wa chumvi unatakiwa kupunguzwa kama ambavyo uvutaji sigara unavyotakiwa. Tafiti za kitaalamu zinaonyesha kwamba mabara ya Afrika na Asia, yamefanikiwa kuzingatia ushauri wa kupunguza matumizi ya chumvi zaidi ikilinganishwa na mabara mengine ulimwenguni. Kwa mujibu wa tafiti hizo, hali hiyo ya mabara ya Afrika na Asia kufanikiwa kuzingatia ushauri wa kupunguza ulaji wa chumvi, imeweza kuzuia vifo vya takriban watu 92,000 kwa mwaka katika mabara hayo, vifo ambavyo vingetokana na ulaji mwingi wa chumvi. Kwa mfano, utafiti uliofanywa mwaka 2012 na Dk Derin Balogun anayeongoza kampeni ya kuzuia maradhi ya moyo na shinikizo la damu duniani, ulibainisha kwamba, hoteli nyingi za Waafrika na watu weusi jijini London, Uingereza, hupika vyakula vyenye chumvi nyingi zaidi. Kwa mujibu wa Dk. Balogun, gramu 12 zilipatikana katika wali na maharagwe, gramu 8.6 ndani ya wali maarufu kwa jina la 'Jollof' kutoka Afrika Magharibi, wakati gramu 19 iligundulika kwenye mikate. Hii ni chumvi zaidi ya gramu tano, zinazotakiwa kwa mtu mzima kutumia kila siku. Si vibaya ukifahamu kwamba chumvi ya asili hupatikana pia ndani ya vyakula vya asili vyenye madini ya Sodium kama vile mayai, nyama na hata baadhi ya vyakula vinavyotokana na maziwa. Mayai kwa mfano, yana miligramu 30 za Sodium. Kwa wale wanaopendelea kula vyakula vinavyopikwa nje ya nyumba zao, kama vile katika hoteli na kwenye migahawa, wanapaswa kuwa waangalifu mno kwa kuwa vyakula vya ‘fast food’ ni vyenye kiwango kikubwa cha chumvi na mafuta pia. Vyakula kama vile chizi, soseji, sosi ya soya na achari mbalimbali ni vyenye kutengenezwa kwa kutumia kiwango kikubwa cha chumvi. Lakini pia chumvi hutumiwa katika kuhifadhi baadhi ya vyakula vya makopo na maboksi. Elimu kama hii ya faida na madhara ya chumvi ni muhimu kwa Serikali, kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuipatia kipaumbele kwa kutoa kwa wananchi wake, kwa faida ya taifa na watu wake. Ipo haja kwa jamii nzima ya Watanzania kuelimishwa vya kutosha kuhusu faida na madhara ya chumvi katika mwili mwa mwanadamu kuliko ilivyo sasa ambapo wananchi wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu ulaji wa chumvi.

Yafahamu Magonjwa Sugu ya Njia ya Hewa, Chanzo chake na jinsi Kuishi nayo

Magonjwa Sugu ya Njia ya Hewa ni magonjwa yanayoathiri njia za hewa pamoja na sehemu nyingine zinazohusiana na mapafu, kama vile magonjwa ya Pumu, Kufungana kwa njia za pumzi (Chronic Obstructive Pulmonary Disease-COPD), ugonjwa wa mapafu unaotokana na kazi (Occupational Lung Disease), kupanda kwa shinikizo la damu kwenye Mapafu (Pulmonary Hypertension) na kadhalika. Magonjwa haya, mara nyingi huathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa hewa na kuzuia kiasi cha hewa inayotoka na kuingia kwenye mapafu, kwa mfano ugonjwa wa Pumu. Hali hii humfanya mgonjwa apumue au kuvuta hewa kwa shida, hasa pale anapokuwa mgonjwa. Magonjwa haya huweza kusababisha kuwepo kwa makohozi katika njia ya hewa, hivyo kusababisha maambukizi mengine. Kutokana na Shirika la Afya Duniani (WHO), watu milioni 235 duniani kote wanasumbuliwa na ugonjwa sugu wa Pumu, huku watu milioni 64 wakitajwa kusumbuliwa na magonjwa sugu ya kufungamana kwa njia ya Pumzi (COPD). Kwa mujibu wa WHO, takriban asilimia 90 ya vifo vinavyotoakana na magonjwa hayo, hutokea katika nchi zilizo na uchumi duni na wa kati, Tanzania ikiwa mojawapo. Watu wengi hudhani kwamba mtu anapokuwa mwembamba kupita kiasi na akawa na uzito kidogo, basi mtu huyo atakuwa na ugonjwa wa Ukimwi. Wanaodhani hivyo, hawajui kwamba magonjwa sugu ya njia ya hewa, nayo yanaweza kumsababishia mtu akakonda na kupungua uzito pia. Hali hiyo hutokea kutokana na ukweli kuwa magonjwa hayo ya njia ya hewa, humfanya mgonjwa atumie nguvu nyingi wakati wa kupumua kuliko mtu asiyekuwa na magonjwa hayo. Matumizi makubwa ya nguvu wakati wa kupumua, humfanya mgonjwa asiwe na nishati ya akiba ambayo huhifadhiwa mwilini, hivyo kufanya mtu kuwa mnene. Lakini pia unene uliokithiri, unaweza kusababisha magonjwa mugu ya njia ya hewa. Ni nini chanzo cha magonjwa sugu ya njia ya hewa? Magonjwa Sugu ya Njia ya Hewa, mara nyingi husababishwa na kuharibika kwa njia ya hewa katika mapafu. Uharibifu huo wa njia ya hewa huweza kutokana na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugolo; kuvuta hewa yenye sumu au vumbi kutoka viwandani, uchafuzi wa hewa ya ndani mfano kwa kutumia jiko la utambi na mafuta ya taa; uchafuzi wa hewa ya nje kutokana na vumbi au poleni ya maua na unene uliokithiri kiwango. Anayesumbuliwa na ugonjwa sugu wa njia ya hewa azingatie nini ili aweze kuishi? Mgonjwa wa ugonjwa sugu wa njia ya hewa anashauriwa kuzingatia ushauri wa daktari na matibabu yake, kufuata kanuni za mtindo bora wa maisha, kuepuka visababishi kama vile vumbi, barafu na harufu, kuhakikisha mazingira na nyumba anaoishi ni safi muda wote, na zaidi pia iwe na madirisha yanayoruhusu mzunguko wa hewa. Aidha, wagonjwa wa magonjwa hayo wanashauriwa kula mlo kamili na vyakula vya aina mbalimbali ili wapate virutubishi vyote vinavyohitajika kwa afya zao. Inashauriwa kula zaidi matunda freshi, mbogamboga zenye rangi ya kijani, matunda yenye rangi ya njano kama vile ndizi, papai, embe, mapera na kadhalika. Lakini pia, wanashauriwa kula vyakula vyenye makapi mlo kwa wingi ili kusaidia mfumo wa kusaga chakula kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa uchafu tumboni kwa urahisi. Hali hii huwasaidia kuweza kupumua kwa urahisi. Ikumbukwe kuwa mgonjwa wa aina hiyo anatumia nguvu nyingi wakati wa kupumua, hivyo basi anahitaji kula chakula cha kutosha ili kumpatia nguvu za kutosha. Ni vizuri kula milo midogo midogo mara kwa mara, ikiwa ni pamoja nakupunguza matumizi ya chumvi ili kuepuka maji kujikusanya mwilini na kusababisha kupumua kwa shida. Ni muhimu pia kuepuka uzito uliozidi kwa sababu unene huongeza tatizo la kupumua. Je, mgonjwa wa mugonjwa sugu wa njia ya hewa anaruhusiwa kufanya mazoezi? Mazoezi ya mwili yana faida nyingi kiafya. Baadhi ya faida hizo ni kuimarisha mapafu na moyo. Ili kuviwezesha viungo hivyo muhimu katika mwili wa mwanadamu vifanye kazi kwa ufanisi, mazoezi ni muhimu sana. Aidha, mazoezi husaidia kuimarisha misuli ambayo hutumika wakati wa kupumua. Kwa hiyo, mgonjwa wa magonjwa sugu ya hewa anaruhusiwa kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi ni sehemu ya matibabu yake. Mgonjwa anapaswa kujitahidi mara kwa mara kufanya mazoezi, kwa kuanza mazoezi ya taratibu kwa kadri mwili wake unavyoweza kustahimili, na kisha kuongeza hatua kwa hatua. Hata hivyo, inashauriwa mgonjwa anayefanya mazoezi, pindi asikiapo maumivu kifuani au kushindwa kuhimili mazoezi hayo, punguza kasi ya mazoezi hayo na fanya kwa taratibu kadri iwezekanavyo.

HATARI: Vimelea vipya vya Kisonono Visivyotibika kama Virusi vya Ukimwi vyagundulika

WAKATI dunia ikipalangana kutafuta dawa ya kutibu ugonjwa wa Ukimwi, imeripotiwa kubainika kwa vimelea vipya vya ugonjwa wa Kisonono, ambavyo havisikii dawa za ugonjwa huo zilizokuwa zimezoeleka ulimwenguni kama tiba sahihi ya maradhi hayo, hivyo ugonjwa huo sasa sasa kutajwa kuwa hatari sawa na Ukimwi. Taarifa mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO), inaeleza kwamba kuna aina mpya vimelea vya ugonjwa wa kisonono vinavyoendelea kusambaa kwa kasi duniani, ambavyo vinahimili dawa zilizokuwa zinatumika kutibu ugonjwa bila kudhulika. Kwa mujibu wa WHO, vimelea hivyo vipya havisikii dawa, hivyo baadhi ya dawa zilizokuwa zikitumika huko nyuma, zimekuwa hazina tena athari kwa vijidudu vipya hivyo. Tayari nchi nyingi duniani zimeripotiwa kukumbwa na usungu wa kisonono hata pale mgonjwa anapopatiwa tiba sahihi ya Antibiotiki (Viuasumu) za jamii ya Sefalosporini na kadhalika, zikiwemo Hongkong, Australia, Ufaransa, Japan, Norway, Sweden na Uingereza. Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinadaiwa kuonyesha usugu dhidi ya dawa zote za Antibiotiki zinazotumiwa kuviangamiza, zikiwemo dawa hizo za jamii ya Sefalosporini, ambazo WHO inazitaja kama dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono. Dk. Manjula Lusti-Narasimhan, kutoka Kitengo cha Afya ya Uzazi na Utafiti cha WHO, amekaririwa akisema: “Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidi ya Antibiotiki (Viuavijasumu) jamii ya Sefalosporini viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway." Daktari huyo hakukomea hapo, bali anasema katika miaka michache ijayo, aina hii mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono, huenda ikawa sugu kwa dawa zote ambazo zinapatikana kwa sasa ulimwenguni. Dk. Manjula anasema: “Ugonjwa sugu wa kisonono si tatizo la Bara la Ulaya au Afrika pekee, bali ni tatizo la dunia nzima. Lazima tahadhari zichukuliwe mapema. Upo uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono kusambaa kwa haraka duniani kote bila kugundulika. Hii inatokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu mzuri wa wagonjwa wake.” Baadhi ya Wanasayansi wa magonjwa hayo ya zinaaa wanaamini kwamba matumizi holela ya dawa aina ya Antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa huo kubadilika na kuzoea mazingira mapya, ndicho chanzo kikuu cha ugonjwa huo kwa sasa kuwa sugu. Kwa mujibu wa wanasansi hao, ugonjwa wa kisonono ambacho si sugu kilicho kwenye shingo ya kizazi (Cervix), Urethra na Puru, hutibiwa kwa Antibiotiki (Kiuavijasumu) jamii ya Sefalosporini, ambapo mgonjwa hupewa dozi moja ya dawa hizo pamoja na dawa aina ya Macrolide kama vile Azithromycin, na za jamii ya Penicillin kama vile Doxycyclin kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Chlamydia. Mara nyingi kwa wagonjwa walio na umri wa chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Mgonjwa lazima afuate masharti na ushauri wa daktari kabla hajatumia dawa hizo, kwa kuwa dawa nyingi huwa na madhara kwa wajawazito kwa mfano Doxycyclin. “Kawaida ushauri nasaha hutolewa kwa washirika wote wawili wa ngono. Na ni vizuri wote wawili watibiwe hata kama mmoja wao hatakuwa na dalili za ugonjwa huu wa kisonono,” wanasema Watafiti na Wanasayansi kuhusu tiba sahihi ya ugonjwa huo. Namna ya kujikinga na ugonjwa huo mpya wa kisonono Utafiti wa wanasayansi waliobobea katika magonjwa ya binadamu, wanasema kwamba mtu anaweza kujikinga na ugonjwa wa kisonono kwa kuwa mwaminifu katika ndoa na kujiepusha vitendo vya zinaa na uasherati. Aidha, mtu anaweza kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuchukua tahadhari na kuzungumzia juu ya ugonjwa huo kwa mshirika wake wa ngono pindi mmoja wapo anapojibaini kuwa na hali yenye dalili zote za ugonjwa ili wote kwa pamoja waweze kutibiwa na kupata ushauri wa daktari mapema. Njia nyingine ya kujikinga ni kuepuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono au kujenga tabia ya kutumia mipira ya kiume (Kondomu) wakati wa kujamiiana. Kwa upande wa wanawake wajawazito ni muhimu kuhudhuria kliniki mapema ili waweze kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka iwapo watagundulika kuwa na ugonjwa huo wa zinaa au ugonjwa mwingine wowote. Kwa mujibu wa WHO, wanawake wajawazito wanatakiwa wajifungulie katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya ili kama watoto wanaozaliwa watabainika kuathirika kwa ugonjwa huo wa kisonono waweze kupata matibabu ya mapema mara tu baada ya kuzaliwa hivyo kuwaepusha na uwezekano wa kupata upofu. Kutokana na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo mpya wa kisonono, kila nchi duniani, kupitia Serikali zao na madaktari wao, zinapaswa kuongeza umakini katika ufuatiliaji wa aina hii mpya ya ugonjwa wa kisonono kwa sababu ugonjwa huo una madhara makubwa kwa afya ya binadamu kama vile kusababisha ugumba kwa wanawake, utasa kwa wanaume, upofu, moyo, uvimbe, ubongo na homa ya mapafu. Takwimu zilizopo kutoka WHO, zinaonyesha kwamba kisonono ni ugonjwa hatari kwa usalama wa binadamu, hivyo muda si mrefu ugonjwa huo unaweza kutangazwa kama moja ya majanga makubwa ya dunia, kama hatua madhubuti na haraka hazitachukuliwa kwa kila nchi. Kutokana na hali hiyo, WHO imezitaka nchi zote duniani kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake, pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za Antibiotiki hadi pale taarifa kamili za ugonjwa huo zitakapojulikana. SambazaTweet about this on Twitter2Share on Facebook8Share on Google+0Share on LinkedIn0Email this to someonePrint this page

Dalili za Ugonjwa wa Uvimbe wa Tezi za Uzazi kwa Wanawake na Tiba yake

Wanawake wengi wanavyoteseka na tatizo la kutoshika ujauzito bila ya kujua sababu yake pia ni nini. Moja ya sababu ya kutoshika ujauzito, ni ugonjwa wa Sisti au Nziba unaopatikana kwenye Ovari za uzazi (Ovarian Cyst). Katika makala haya ya sehemu ya pili tutaangazia tena dalili na viashiria vya kwanza kabisa vya ugonjwa huu wa Sisti/Nziba. Dalili na viashiria vya kwanza kabisa vya ugonjwa wa Sisti/Nziba kwenye Tezi za Uzazi za Mwanamke ni maumivu makali ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, ambapo maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja. Lakini pia, mwanamke anaweza kupata usumbufu na kutojisikia vizuri kwenye maeneo ya chini ya kitovu, kwenye nyonga, uke, kwenye mapaja na mgongoni upande wa chini kiunoni. Dalili nyingine ni maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati mwanamke anapokuwa kwenye siku zake, maumivu ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya kiunoni. Kwa kawaida mumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi. Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kujamiiana. Kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni. Ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo, yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo. Mabadiliko ya haja kubwa, kwa maana ya kupata haja kubwa kwa shida sana kutokana na presha kwenye maeneo ya nyonga; nywele kukua kwa kasi na kuongezeka kuota kwa nywele kwenye uso au sehemu nyingine za mwili. kuumwa kichwa, kuongezeka uzito, maumivu ya kwenye mbavu, kutokewa na uvimbe chini ya ngozi na kuvimba mara kwa mara; maumivu kwenye matiti na kuapata hedhi isiyokuwa na mpangilio maalumu na kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba. Mwanamke mwenye dalili na viashiria hivi afanye nini? Kwanza kabisa ni kufanyiwa kipimo cha mawimbi ya sauti ndani ya uke (Endovaginal Ultrasound). ambacho hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua kama kuna uvimbe wowote kwenye Ovari na uvimbe huo ni wa aina gani au atajua kama ni maji tu (Fluid filled sac), au ni maji pamoja na mchanganyiko wa ute mzito, au ni ute mzito pekee. Kipimo kingine kinachoweza kuchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi ni kipimo cha mawimbi ya sauti kutoka kwenye nyonga hadi kwenye fumbatio (Pelvic Abdominal Ultrasound) ambayo ni Ultrasound ya kawaida. Hii husaidia kujua aina ya uvimbe uliopo kwenye tezi za uzazi (Ovari) za mwanamke. Vipimo vingine vinavyoweza kuonyesha uvimbe kwenye Ovari ni pamoja na Computerized Tomography (CT) Scan na Magnetic Resonance Imaging (MRI) Scan. Matibabu ya Ugonjwa wa Tezi za Uzazi za Mwanamke Matibabu ya Sisti/Nziba kwenye Ovari yanategemea sana umri, aina na ukubwa wa uvimbe pamoja na dalili anazohisi mgonjwa. Mgonjwa anaweza kushauriwa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ili kupunguza hatari ya kupata Sisti/Nziba kwenye Ovari. Ni muhimu kufahamu kwamba vidonge vya uzazi wa mpango, mbali na kuzuia upatikanaji wa mimba zisizokuwa na mpango, hupunguza pia hatari ya kupata Kansa au Saratani kwenye Ovari za Uzazi wa Mwanamke. Kwa hiyo, matiba ya magonjwa haya yanaweza kuhusisha vipimo vya damu kama CA-125 ili kuangalia uvimbe huo kama ni Saratani au ni uvimbe wa kawaida tu. Uvimbe kama haupungui na unasababisha maumivu makali sana, mgonjwa anaweza kushauriwa kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo. Kama mgonjwa atalazimika kufanyiwa upasuaji, uvimbe uliotolewa unaweza kupelekwa kwa mtaalam wa Patholojia kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kupata bainisho la mwisho la ugonjwa (Final Diagnosis). Endapo uchunguzi utaonyesha kwamba uvimbe huo ni wa Saratani, basi Daktari atamshauri mgonjwa kutolewa kwa viungo vyote vya uzazi (Total Hysterectomy) ili kuzuia Saratani kutosambaa kwenye viungo vingine. SambazaTweet about this on Twitter0Share on Facebook5Share on Google+0Share on LinkedIn0Email this to someone

Wanaotoa Mimba chini ya Miaka 18, hatarini kupata Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi

WASICHANA wanaopata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 18 pamoja na wenye tabia ya kutoa mimba mara kwa mara, wametajwa kuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Mbali na kundi hilo, pia watumiaji wa dawa za kulevya, watu wenye magonjwa ya zinaa, wanawake wanaozaa mara kwa mara na wanaume wasio tahiriwa nao wapo katika hatari ya kupata aina hiyo ya saratani. Mshauri wa masuala ya Afya ya Uzazi, Leojin Mnzava, ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibaha, amebainisha hayo katika mafunzo ya kuwapatia elimu hiyo ya Afya ya Uzazi wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wilayani humo na kuwa tayari wameanza kutoa elimu ya ugonjwa wa Saratani ya shingo ya kizazi kwa ajili ya kuokoa maisha ya wanafunzi walio na tabia ya kufanya mapenzi kabla ya wakati. Amesema kwamba saratani ya shingo ya kizazi, ni hatari kuliko magonjwa mengine kama vile Ukimwi na Malaria, hivyo wanawake wanapaswa kuwa makini na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha au kuchochea magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa huo. Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Asasi ya Maendeleo ya Wanawake ya INUKA, Gaudience Msuya, yenye makao yake makuu Jijini Dar es Salaam, amesema wametoa mafunzo kwa walimu 40 waliopo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, ambayo yamelenga kuwakumbusha walimu visababishi vya saratani ya shingo ya kizazi ili waielimishe jamii wakiwemo wanafunzi. Lindi yatajwa kuongoza Saratani za Matiti na Shingo ya kizazi Wakati huo huo, Mkoa wa Lindi umetajwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake waliogundulika kuwa na saratani ya matiti na shingo ya kizazi kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya kutambua dalili za ugonjwa huo, ambao kama ukitambuliwa mapema unatibika. Daktari Faridi Ally kutoka Hospitali ya Sokoine iliyoko Mkoani Lindi, amebainisha hayo wakati wa mahojiano na FikraPevu na kwamba wataalamu kutoka katika hospitali hiyo wamekwishaanza kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya 300, juu ya kutambua dalili za ugonjwa wa saratani na kusisitiza umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu cha kutibu maradhi hayo. Mkuu wa mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza, amesema mipango ya Serikali ya mkoa ni pamoja na kuwa na kitengo maalumu cha kutibu maradhi hayo na kwamba kwa kuanza wameanza kutoa elimu ili kupunguza tatizo kabla ya mipango hiyo haijakamilika. Saratani ya kizazi ni nini? Ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizoko kwenye ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi. Chanzo cha ugonjwa huo ni kirusi kiitwacho 'Human Pailloma Virus' na huambukizwa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye maambukizi hayo. Aidha, dalili za ugonjwa ugonjwa huo ni pamoja na kutokwa na majimaji au uchafu usio wa kawaida ukeni, kutokwa na damu ukeni wakati ambao mwanamke hayuko kwenye hedhi pamoja na maumivu makali wakati wa kujamiana. Tafiti mbalimbali zilizofanywa na taasisi za Afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) zimebainisha kwamba tabia hatarishi inayopelekea kupata magonjwa haya ni pamoja na kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18), uvutaji wa sigara, kuzaa mara kwa mara, matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula, kuwa na wapenzi wengi au kujamiana na mtu mwenye wapenzi wengi.

Unataka kutumia Vidonge vya Uzazi wa Mpango Kuzuia Mimba? Jiandae na Madhara 10 haya

Vidonge vya Uzazi wa Mpango, ni moja ya njia inayopendekezwa na Wataalamu wa Mpango wa Uzazi katika kuzuia mimba. Hata hivyo, vidonge hivyo vinaweza kutimiza malengo hayo ya mpango huo ikiwa tu vitatumiwa vizuri na kwa usahihi, kwa sababu tafiti zilizopo, zinaonyesha kwamba asilimia nane (8%) ya wanawake hupata mimba zisitarajiwa kila mwaka, huku wakiwa katika mpango huo kutokana na baadhi yao kujisahau kumeza vidonge hivyo. Kwa mujibu wa tafiti, vidonge hivyo vya mpango wa uzazi vikitumiwa vizuri, kwa kuhakikisha muda wa matumizi yake unakuwa ule ule, ni mwanamke mmoja pekee kati ya 100 anayeweza kupata mimba isiyotarajiwa ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi ya dawa hizo. Hadi sasa kuna aina kuu mbili tu za vidonge vya uzazi vinavyotumiwa na wanawake katika wa mpango huo, ingawa aina zote hizo zina vichocheo (hormons). Aina hizo kitaalamu zinaitwa Estrogen na Progesteron. Estrogen ni aina ya kichocheo kinachotengenezwa na uterasi/kizazi, kinachosaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kwa kuongoza ukuaji wa kuta za uterasi kwenye sehemu ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Kwa upande wake, Progesteron, hiki ni kichocheo cha kopasi luteamu ya ovari, kinachosaidia kuanzisha mabadiliko katika endometriumu baada ya ovulesheni. Ingawa katika aina hiyo mbili ya vidonge, kuna vingine vina kichocheo cha aina moja tu, kwa maana ya ama Estrogen au Progestron, huku vingine vikiwa na vichocheo vyote viwili hivyo, lakini vidonge vyote hivyo ni salama, na vinafanya kazi kwa kufanya ute mzito kwenye shingo ya mji wa mimba na kuzuia kupevuka kwa yai, hivyo kuzuia mimba kwa kiwango cha asilimia 99. Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza pia kutumika kama tiba ya kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuzuia maumivu makali wakati wa hedhi, kutibu chunusi pamoja na kupunguza hatari ya magonjwa katika via vya uzazi, ambayo hayatokani au kusababishwa na magonjwa ya ngono. Hata hivyo, pamoja na usalama wa vidonge hivyo katika kufanya kazi yake hiyo ya kuzuia mimba na tiba kwa magonjwa hayo, vidogo hivyo vinaweza kumsababishia athari za kiafya mwanamke kama havitumiki katika mpangilio sahihi. Athari kuu 10 zinazoweza kusababishwa na vidonge hivyo ni pamoja na kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi ya kawaida. Kwa mujibu wa wataalam wa mpango huo, athari hiyo huweza kuwapata asilimia 50 ya wanawake wote wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango. Hali hii huweza kuwatokea ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza matumizi ya dawa hizi. Kwa ujumla, hali hiyo huweza kukoma kwa zaidi ya asilimia 90, pindi mwanamke anapoanza kutumia pakti ya tatu ya dawa hizo katika kipindi hicho cha kutokwa damu ukeni. Mwanamke anapotokewa na hali hiyo kwa mfululizo wa siku tano au zaidi baada ya kumaliza siku zake za kawaida za hedhi, anashauriwa kuwasiliana na mhudumu wa afya wakati akiendelea kutumia dawa hizo. Athari ya pili, ni kujisikia kichefuchefu. Mara nyingi hali hiihumtokea mwanamke mwanzoni tu baada ya kuanza kumeza vidonge vya uzazi wa mpango, ingawa hali hii inaweza kukoma baada ya siku chache. Inashauriwa pia kwa mwanamke anayepatwa na hali hii ya kichefuchefu kuwasiliana na mhudumu wa afya kama ataona hali hiyo inazidi. Matiti kujaa au kuwa na maumivu, ni athari nyingine inayoweza kusababisha na matumizi ya vidonge hivyo. Hali hii huweza kumpata baada ya kuanza kutumia vidonge hivyo, na huweza kukoma ndani ya wiki moja tu. Hata hivyo, inashauriwa kwamba ikiwa matiti hayo yatatokwa na uvimbe au maumivu yasiyoisha, ni muhimu kutafuta tiba kwa wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya kinywaji chenye kafeini na chumvi na kuvaa brauzi isiyobana matiti. Maumivu ya kichwa ni athari nyingine inayoweza kumtokea mwanamke, ingawa pia kuumwa kichwa kunaweza kuwa na dalili za magonjwa mengine. Hata hivyo, kama itatokea maumivu hayo ya kichwa yakaanza tu mara baada ya kumeza vidonge hivyo, hiyo itakuwa ni dalili ya athari mojawapo na ni vyema kutoa taarifa kwa mhudumu wa afya. Vidonge vua uzazi wa mpango huweza pia kuongezeka uzito wa mtumiaji, ingawa tafiti nyingine zimeshindwa kuthibitisha uhusiano kati ya vidonge hivyo na mabadiliko ya uzito wa mtumiaji. Aidha, baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo la maji kuganda kwenye matiti na maeneo ya nyonga baada ya kutumia vidonge hivyo. Mabadiliko ya hisia huweza pia kumtokea mwanamke anayeanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Inashauri kwamba pindi mwanamke anapoona dalili hii, ni muhimu kumjulisha mhudumu wa afya ili kuweza kujadili ni jinsi gani ataweza kutumia dawa hizo, kwa sababu dalili hii ni mbaya kiafya kwa mtu mwenye historia ya ugonjwa wa Kushuka Moyo (Depression). Adhari nyingine ya dawa hizi ni kutokwa na uchafu ukeni. Baadhi ya wanawake, mara tu baada ya kutumia vidonge hivi hutokwa na uchafu ukeni, ikiwa ni pamoja na kupatwa na uwezekano wa kupungua au kuzidi kwa ute wakati wa tendo la ndoa. Ni muhimu sana mwanamke anapobaini dalili hizi, kuonana na mhudumu wa afya ili kubaini kama hali hiyo imesababishwa na athari ya vidonge au kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Wanawake wengine huweza kujikuta wakikosa siku zao za hedhi baada ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Ingawa ugonjwa wa msongo wa mawazo (Stress), magonjwa, mchoko wa safari unaweza kusababisha hali hii, lakini inashauriwa kupima kama mtu amaepatwa na ujauzito hata kama anatumia vidonge hivi kama itatokea kukosa hedha katika mazingira tata. Kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni athari nyingine inayoweza kumkuta mwanamke anayetumia vidonge vya uzazi wa mpango kutokana na vichocheo vilivyomo ndani ya dawa hizo, ingawa pia magonjwa kama ya kisukari, shinikizo kubwa la damu na kadhalika yanaweza pia kuchangia tatizo hilo. Athari ya 10 na ya mwisho kwa wanawake wanaotumia vidonge hivyo, ni mabadiliko ya taswira ya kitu anachokiona mbele yake, hasa kwa wanawake wanaovaa miwani ya macho. Kwa kuwa macho ni moja ya eneo muhimu la ufahamu kwa mwanadamu, hali hii inapowapata wanawake, inashauri kuonana mara moja na daktari wa macho pindi tu dalili hizi zinapoanza kujitokeza. Ni tahadhari gani mwanamke anatakiwa kuchukua kabla na baada ya kuanza matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango? Kwa mwanamke mzazi, hairuhusiwi hata kidogo kuanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ndani ya wiki tatu tu baada ya kujifungua mtoto au ikiwa atakuwa ananyonyesha mtoto mwenye umri wa chini ya miezi sita. Aidha, ikiwa mwanamke amefanyiwa upasuaji mkubwa wa aina yoyote katika siku za karibuni, au kama mwanamke husika ni mvutaji wa sigara na ana umri wa zaidi ya miaka 35, haruhusiwi kutumia vidonge hivyo, kama ambavyo pia haruhusiwi kufanya hivyo mwanamke mwenye historia ya ugonjwa wa ini, manjano, moyo, saratani ya matiti, tumbo la uzazi pamoja na shinikizo la damu linalobadilikabadilika kila wakati kwa viwango vya 140/90 au zaidi, na au kama ana historia ya maumivu makali ya kichwa.

Madhara ya Heroin kwa wajawazito

WAKALA wa maabara ya mkemia wa serikali, ndiyo mamlaka yenye jukumu hapa nchini ya kufanya uchunguzi wa kitaalam ili kubaini, kutambua na kuthibitisha aina na madhara ya dawa za kulevya. Mamlaka hiyo inaeleza kuwa, Heoin ni aina ya dawa ya kulevya inayotokana na mmea unaojulikana kama Oppium poppy. Kilimo cha mmea huo hufanyika kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Afghanistani. Vile vile mmea huo unalimwa kidogo nchini Misri. Dawa hii hupambaza mfumo wa fahamu na kusababisha mtu kupata usingizi, kupungua kwa mawazo na maumivu makali. Majina mengine ya Heroin ni Unga, Brown Sugar, Ngoma, ubuyu, Mondo, Dume, Farasi na Ponda. Kwa mujibu wa kijarida cha wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali, idara ya huduma za sayansi ya makosa ya jinai(Forensic Science Services), kinaainisha madhara wayapatayo wajawazito wanaotumia dawa aina hii. Madahara hayo kwa wajawazito ni pamoja na upungufu wa damu mwilini, mimba kuharibika, kujifungua watoto njiti, kujifungua watoto ambao hufariki kabla ya kutimiza miaka mitano na watoto kupata matatizo ya kiafya ikiwemo kuchelewa kukua kiakili. Mengini ni kuleta mabadiliko ya hedhi kwa wanawake na hujenga hali ya uteja kwa haraka sana kuliko dawa zingine za kulevya. Madhara ya kijamii Madhara yatokanayo na utumiaji wa dawa za kulevya kwa jamii ni pamoja na kuvunjika kwa ndoa, kutoweka kwa amani katika jamii ikiwemo ongezeko la fujo na uhalifu, matatizo ya mwajiri na mwajiliwa na ongezeko la mzigo kwa jamii na vyombo vya usalama na taifa kwa ujumla. Madhara ya jumla kwa watumiaji wa dawa hii ni kuharibika kwa mfumo wa fahamu, kapata njozi, kupata magonjwa ya moyo, ini, kifua kikuu na kupumjua, kushuka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Kwa watumiaji wa Heroin kwa njia ya kujidunga wanapata matatizo ya kuambukizana VVU kwa kuwa baadhi yao hushirikiana sindano, kuzubaa na kupunguza uwezo wa kufanya kazi, kichefuchefu, kizunguzungu na dozi kubwa hupelekea kifo.

Yafahamu madhara ya Mirungi

MIRUNGI ni aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unevunyevu na milima yenye urefu wa kati ya futi 4000 hadi 9000. Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika mikoa ya Arusha, Kilimajaro, Manyara na Tanga. Hata hivyo kiasi kikubwa cha mirungi itumikayo nchini huingizwa isivyo halali kutoka nchini Kenya. Mirungu hujulikana kwa majina mengi kama vile Miraa, Mbaga, Mogoka, Veve, Bomba na Kashamba. Kwa mujibu wa wakala wa Maabara ya mkemia Mkuu wa Seriali ya Tanzania, Mirungi ina kemikali inayojulikana kama “Cathinone”, ambayo mtumiaji akitumia hukosa hamu ya kula. Madhara mengine kwa mtumiji wa Mirungi ni kutokwa na vidonda vya mdomoni na tumboni, kukosa choo, kupungukiwa maji mwilini, kupata shinikizo la damu, kupungukiwa nguvu za kiume, mwili kuwasha, kupata maumivu makali ya kichwa na kuharibika ini. Sheria ya dawa za kulevya ya mwaka 1995, inasema kuwa, ni kosa la jinai, kutumia, kuhamasisha matumizi, kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na mirungi.

Cocain na madhara kwa mtumiaji na jinsi ya kumsaidia

COCAINE ni dawa ya kulevya inayotengenezwa kutokana na mmea wa coca, unaostawishwa katika nchi za Amerika ya kusini. Dawa hii ipo katika kundi la kichangamshi kikali ambacho huathiri mfumo wa ufahamu. Cocaine huwa katika unga mweupe au katika hali yam awe madogo madogo. Majina ya mtaani Cocaine hujulikana kwa majina mengi ikiwemo; Unga, White sugar, Keki, Big C, Bazooka, Snow, Keki, Unga mweupe nk. Kinachotokea baada ya kutumia Cocaine. Kwa mujibu wa kijarida kilichotolewa na ofisi ya wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali na kupatikana katika banda la Tume ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya nchini, katika maazimisho ya kupinga dawa za kulevya kitaifa yaliyofanyika Jijini Mbeya June 26, mwaka huu kinaeleza. Kijarida hicho kinaeleza kuwa, wenyeji wa Amerika ya kusini, hutumia cocaine kwa kutafuna. Aidha, unga mweupe wa cocaine, hutumika kwa njia ya kuvuta kwa kutumia pua au kunusa. Cocaine aina yam awe madogo madogo hutumika kwa njia ya kuvuta. Mara baada ya kutumia cocaine kwa kiwango kidogo, dalili zifuatazo zinaweza kuonekana. Dalili hizo kwa mtumiaji ni uchangamfu kupita kiasi, kupungua kwa hamu ya chakula, kupanuka kwa mboni za macho, kukauka koo, kutokutulia, kuwa na mhemuko wa kufanya ngono, kusinyaa kwa mishipa ya damu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Jukumu la maabara ya mkemia mkuu wa serikali Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, unalo jukumu la kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini, kutambua na kuthibitisha aina na madhara ya dawa za kulevya Madhara yatokanayo na matmizi ya kiwango kikubwa cha cocaine. Madhara hayo ni pamoja na njozi/maono yasiyokuwepo, kuchanganyikiwa, kuwashwa mwili, kuwa na hasira za ghafla, hisia za kuwepo vijidudu mwilini, kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo kunakoweza kusababisha kiharusi au kifo, kuongezeka na kupungua kwa mapigo ya moyo ghafla na kutetemeka kwa nguvu kama kifafa. Meneja wa mafunzo kutoka shirika la kifaransa la MDM, lenye makao makuu wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, linaloshughulika na upunguzaji wa athari zitokanazo na matmizi y dawa za kulevya, Damal Lucas, anasema kuwa, cocain inachangamsha mfumo wa fahamu lakini huisha haraka mwilini. Damali anasema dawa hiyo ikiisha katika mwili wa mtumiaji, inasababisha mtumiaji kujisikia vibaya(Alosto) ikiwemo kukosa raha, kusonaneka na kunyongea. Ili kuzuia hali hii, watumiaji wengi huendelea kutimia. Dawa hii ni hatari sana na huleta utegemezi katika kipindi cha muda mfupi baada ya utumiwa. Mtumiaji huweza kuiba,kutapeli, kudanganya na hata kuwa jambazi ili kupata fedha za kununulia dawa hii. Madhara mengine ni mtumiaji kupata madhara ya kisaikolojia yanayoweza kufanya kuwa mkorofi, mkali na mwenye fujo, kukosa ufanisi kazini na kupata matatizo ya kifamilia. Madhara mengine ya kiafya ni kutokwa damu puani, kutokwa na vidonda puani, magonjwa ya ini, kuziba mishipa ya damu, kuharibika mishipa ya fahamu, mchafuko wa damu na kupata majipu na kuharibika kwa moyo na figo. Kama cocaine ikitumika kwa kuvuta au kunusa mfumo wa upumuaji huathirika na kumfanya mtumiaji kushindwa kupumua vizuri, kikohozi cha muda mrefu, maumivu ya kifua na kuharibika kwa mapafu. Matumizi ya cocaine na dawa zingine za kulevya humweka mtumiaji katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU na huongeza uwezekano wa kifo cha mapema. Utamsaidiaje mtumiaji wa cocaine? Kama mmojawapo wa marafiki au mtu wako wa karibu anatumia cocaine, mwambie ukweli kuwa cocaine huathiri ubongo, mwili na hisia zake. Vile vile ajue kwamba anaweza kuwa mtegemezi wa dawa hii na kusababisha kifo. Mwonyeshe unamjali.

BANGI INAVYOINGIZWA KATIKA MAGEREZA

BANGI ni dawa ya kulevya iliyopo kwenye kundi la dawa za kulevya lenye kuleta Njozi (Hellucinogences). Vileta njozi huathiri ubongo na kumfanya mtumiaji kutoa tafsiri potofu ya hisia na kujisikia kama vile yuko nje ya dunia. Mtumiaji wa bangi huzalishwa na kutumiwa kwa wingi barani Afrika kwa sababu hustawi maeneo mengi. Nchini Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini, mkoani Njombe wilayani Makete hustawi zaidi. Wakati Serikali ikiamini kuwa gerezani ni mahala salama hata kuwatunza wanaokamatwa na dawa za kulevya, hali si shwari katika baadhi ya magereza hapa nchini, kutokana na ongezeko la matumizi ya dawa hizo. Baadhi ya askari Magereza, wafungwa na mahabusu katika magereza mbalimbali hapa nchini, wanahusishwa na biashara ya dawa za kulevya ndani ya magereza, imebainika. Uchunguzi uliofanywa kwa miezi miwili sasa, umebaini kuwepo kwa dawa za kulevya katika magereza mengi hapa nchini, hususani Bangi. Baadhi ya askari ambao hawakutaka kutajwa majina yao na vyeo katika Gereza la Ruanda na Songwe mkoani Mbeya, walithibitisha kuwepo kwa uingizwaji wa bidhaa hiyo ambayo inafanyika kwa siri kubwa katika magereza hayo. Biashara hiyo inahusisha baadhi ya askari, wafungwa na mahabusu wenye kesi mbalimbali, wanaokaa muda mrefu gerezani huku kesi zao zikiahirishwa mara kwa mara. Baadhi ya waliowahi kuwa mahabusu wa gereza la Ruanda mkoani Mbeya, wanaeleza kuwa wahusika wakubwa ni baadhi ya wafungwa wanaofanya kazi nje ya gereza, kisha kurejeshwa alasiri na baadhi wanaopelekwa mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi zinazowakabili. Wanasema njia ambazo zinatumika kuingiza dawa hizo gerezani ni kujiingiza katika sehemu ya haja kubwa wakiwa nje ya gereza na wakati wa ukaguzi unapofanyika kwa kila anayeingia gerezani hapo, askari wanashindwa kubaini. “Baadhi ya wafungwa ambao wanakaribia kumaliza muda wao, wanatolewa kwenda kufanya kazi za nje ikiwemo kwenda kukata nyasi za Ng’ombe na kurejeshwa mchana na wale wanaoenda kusaga mashine wanaweka kwenye unga. Hao wana mtandao na wauza bangi uraiani, wanaingia nazo na kufanya biashara ndani ya gereza, mle kuna biashara nyingi” anaeleza mmoja wa aliyekuwa mahabusu katika gereza hilo na kuachiliwa huru hivi karibuni baada ya Mahakama kuona hana hatia. Baadhi ya askari mgambo wanaotumwa kuwachukua mahabusu na kuwapeleka katika mahakama za mwanzo, ambao nao waliomba hifadhi ya majina yao, walikiri kuwepo kwa biashara hiyo ambapo walisema kuwa, biashara hiyo inafanyika kutokana na vipato vidogo vya Mgambo na askari Magereza kutokuwa na mianya ya rushwa tofauti na askari polisi. Mbali na bangi, wanasema kuwa, katika magereza pia kuna uvutaji mkubwa wa sigala ambazo huingizwa kwa njia za haja kubwa kisha kutolewa vyooni na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya sero na nje ya sero bustanini. Wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, idara ya huduma za sayansi ya makosa ya jinai (GCRLA), inataja madhara yanayowakuta watu wanaotumia dawa hii ya kulevya kuwa ni kuwaza, kuona, kusikia na kuhisi vitu kwa namna tofauti au visivyokuwepo, kupata njozi, kuongezeka kwa hamu ya kula, kuwa kama kichaa, kutapika, wasiwasi, hamaki na kupumbaa. Madhara yatokanayo na matumizi ya muda mrefu Madhara hayo ni kupata ugonjwa wa akili, mabadiliko ya maono, hisia na mtizamo yasiyoisha, kuharibika kwa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kukumbuka na kufikiri na kukosa ari ya maendeleo na mabadiliko ya aina yoyote ile. Sheria inasemaje kuhusu bangi Kutumia, kuhamasisha matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifdhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na bangi ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha. Sheria inasemaje kuhusu bangi Kutumia, kuhamasisha matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifdhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na bangi ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha. Mbali na tatizo la Bangi, moja ya matatizo yanayotajwa ni suala la kutumia kwa kubadilishana vitu vyenye ncha kali zikiwemo nyembe. “Nilikamatwa na kupelekwa gerezani mwaka 2011, nikakuta watu wananyolea wembe mmoja ambapo kilichoniuma ni kwamba kuna rafiki yangu aitwaye Jack, alikuwa anaishi na VVU, alinyolea wembe akajikata, akampa jamaa anaitwa Kamugisha akajikata, naye akampa Side, naye akajikata na Side alimpa Chidi akatie kucha naye akajikata, virusi vikasambaa kwa wote”anasema Frank Kaitaba, kijana ambaye alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya Jijini Dar es Salaam na sasa anahudumiwa na shirika la Medecin De Munde la Temekelinalopunguza athari za madawa ya kulevya.. Anasema baada ya hapo akaamua kuwafuata madaktari wa gereza hilo na kuanzisha kikundi cha uelimishaji rika ndani ya gereza na kwamba tangu hapo ndani ya gereza hilo mtu anapotaka kunyoa anampa taarifa kiongozi aitwaye Onyango, ambaye anatoa wembe na kumwamuru nyapala asimamie matumizi ya nyembe.

Tuesday, July 14, 2015

MTAMBUE JUMA NKAMIA KUTOKA UANDISHI WA HABARI HADI NAIBU WAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alimuapishe Juma Nkamia kuitumika Serikali kama Naibu Waziri katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kwa taaluma, Naibu Waziri Nkamia (Pichani) ni mwanahabari ambaye amesomea na kufanya kazi ya habari kwa kipindi kirefu kabla ya kuingia katika Ubunge ambao umemuwezesha kuteuliwa kuwa waziri. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika wizara hiyo, Nkamia alisema anamshukuru Rais Kikwete kwa kumteua na kumpa dhamana hiyo na kuahidi kuwa atasaidiana na Waziri wa wizara hiyo kutimiza majuku ya wizara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya nne. “Kama kiongozi mwenye mamlaka ndani ya wizara hii, nipo tayari kushirikiana na viongozi wenzangu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara zote zinazounda wizara hiyo”, alisema. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaundwa na idara kuu nne za kisekta ambazo ni Idara ya Habari, Idara ya Vijana, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Idara ya Maendeleo ya Michezo. Kwa kuwa tasnia ya habari ni miongoni mwa idara zilizo chini ya wizara hii, Nkamia alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na wadau wa habari ikiwemo kusimamia maslahi ya waandishi wa habari nchini. “Ukitaka kujua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika nchi yeyote ile, jaribu kuvifanya vyombo hivyo kuanzia redio, televisheni na magazeti visifanye kazi hata kwa muda wa saa moja tu uone ni hasara kiasi gani na hatari kiasi gani zitatokea katika nchi ile” alisema Nkamia. Alisema anaheshimu na anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini na atafanya nao kazi vizuri kwa kipindi chote atakachokuwa wizarani hapo. Alisema kuwa anatambua kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira magumu wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo tatizo la “ukanjanja” na lugha mbalimbali zinozotolewa juu yao. Amaeahidi kushirishirikiana na viongozi na wadau wa habari kuhakikisha kinaundwa chombo (bodi) kitakachosimamia maslahi ya waandishi wa habari. Bodi itakayoundwa itasaidia kusimamia tasnia ya habari na kuhakikisha habari zinazoandikwa zitakuwa kwa maendeleo, manufaa na maslahi ya taifa na kuhakikisha inawajengea heshima waandishi wenyewe kwa kazi zao wanazofanya kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na ya nchi. Naibu Waziri Nkamia ametoa rai kwa wadau wote wa habari kushirikiana ili kufanikisha uundwaji wa sheria ya habari. Alisema “Sheria hii ikikamilika itasaidia kuboresha baadhi ya changamoto za wanahabari ikiwemo ajira zao na mafao yao ya sasa na uzeeni”. Nkamia amepewa wadhifa huo baada ya Rais Dkt. Kikwete kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri katika kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki mwanzoni mwa mwezi huu. Nkamia ni mkongwe aliyebobea katika taaluma ya uandishi wa habari akiwa amefanya kazi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Aliajiriwa kwa mara ya kwanza na Redio ya Taifa (Radio Tanzania Dar es Salaam) mnamo Oktoba 10, 1994 kama mwandishi msaidizi. Alifanya kazi RTD kwa muda wa miaka tisa hadi 2003 alipojiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC). Akiwa BBC Nkamia alifanya mambo mengi mazuri yaliyomjengea heshima mwenyewe na taifa. Ikizingatiwa kuwa Nkamia alipenda sana kutangaza habari za michezo, alifanikiwa kutangaza mechi mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Kama mwandishi wa habari za michezo, Nkamia alikuwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutangaza mchezo wa mpira wa miguu wa ligi ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili. Kutokana na umahiri wake katika kutangaza habari za michezo, Nkamia aliaminiwa kutangaza mchezo wa fainali ya ligi ya Uingereza mwaka 2006 kati ya Manchester United na Arsenal na mwaka huo huo, BBC ilimpa tena jukumu la kutangaza mechi ya fainali ya Ligi ya klabu bingwa ya Ulaya kati ya Arsenal na Barcelona. Mwaka 2006 Nkamia alirudi nyumbani Tanzania na kujiunga na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo alifanyakazi kama mwandishi na mhariri hadi 2009. Mwaka 2009 hadi 2010 Nkamia alifanya kazi ya uandishi katika shirika la utangazaji la Sauti ya Amerika (VOA) inayomilikiwa na Taasisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kazi ambayo aliifanya kwa mwaka mmoja. Mwaka 2010 Nkamia alitambua na kuitikia dhamiri yake ya kuitumikia nchi yake katika mambo ya siasa hivyo aliamua kurudi Tanzania kuomba ridhaa ya wana Kondoa Kusini awe mwakilishi wao bungeni na Kamati Kuu ya chama chake, Chama cha Mapinduzi, ikapitisha jina lake kuwa mgombea ubunge wa chama hicho jimboni humo. Nkamia anasema, kwa kuwa alikuwa anafanya kazi na watu, wapo waliomshagaa kuacha kazi ya maslahi zaidi na kurudi nyumbani. Miongoni mwa hao ni Dkt. Shaka Ssali mtangazaji na mmoja wa wanahabari maarufu duniani aliyeuliza Nkamia anafanya nini katika karne yenye changamoto ya ajira duniani kuacha kazi yenye mshahara na maslahi makubwa na kwenda kwenye siasa. Anasema kwake jibu la swali hilo lilikuwa rahisi kuwa ni Uzalendo wa nchi kwanza ndiyo maana aliamua kurudi kutoa mchango wake kwa maendeleo ya watu wake wa Kondoa Kusini na nchi kwa ujumla. Kwa kuzingatia ukomavu na weledi alionao kwenye taaluma ya habari, ndiyo maana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameamini na kumpa dhamana ili asaidiane na Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo, Fenella Mukangara, kuiongoza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Nkamia amechukua nafasi hiyo badala ya Mhe. Amosi Makalla aliyehamishiwa Wizara ya Maji. Wengine waliowahi kushika nafasi ya Naibu Waziri katika wizara hiyo ni Dkt. Makongoro Mahanga, N. Nswanzungwanko, Joel Bendera, Dkt. Emmanuel Nchimbi na Dkt.Fenella Mukangara ambaye sasa ni waziri wa wizara hiyo. Juma Nkamia ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto sita wa familia ya Mzee Selemani Nkamia na Mwanaidi Ndwata. Anatokea eneo la kanda ya Kati katika mkoa wa Dodoma wilayani Kondoa. Ni baba wa familia mwenye mke mmoja Bi Amina na watoto wawili ambao ni Kassi mwenye umri wa miaka 13 anayesoma kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Wavulana Fezza na Hassani mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la pili katika shule hiyo hiyo.

CHAMA CHA MAPINDUZI NA HISTORIA YAKE.

Chama cha Mapnduzi CCM kinaendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya chuki na msambaratiko wa umoja wa kitaifa, amani na mshikamano. Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania. CCM ilizaliwa 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume. Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

MAUMIVU YA TUMBO KWA WANAWAKE (Natural home remedies for Endometriosis)

Endometriosis: • Endometriosis is a common health disorder affecting women • The condition can cause problems in conceiving Symptoms to look for: • Painful periods • Painful cramps during menstruation • Pain in the lower abdomen • Pain during sexual intercourse • Painful bowel movement Causes: • Certain cells, which are supposed to grow in the womb lining, start to grow outside the uterus, leading to this condition Natural home remedy using milk and asparagus powder: 1. Take 1 glass of warm milk 2. Add 2 tsp of Indian asparagus powder 3. Mix well 4. Drink 2 times a day Natural home remedy using the Ashoka tree's bark: 1. Crush the bark of an Ashoka tree to powder, commonly available at ayurvedic stores 2. Take 2 tbsp of this powder 3. Mix it in 250 ml of water 4. Heat this water till only half the liquid remains 5. Strain the liquid 6. Drink 2 times a day Natural home remedy using flax seeds: 1. Take 4 tbsp of flax seeds 2. Soak them in 1 cup of water overnight 3. Strain and drink this water the next morning Tips: • Drink pineapple juice to quicken the healing process - See more at: http://mtsimbe.blogspot.com/2013/06/maumivu-ya-tumbo-ya-wanawake-natural.html#sthash.EMYO14go.dpuf

TIBA YA KUTOKA DAMU KWENYE FIZI

Pyorrhea: • Pyorrhea is an advanced stage of gum disease • It's a painless disease and hence goes undetected Symptoms to look for: • Dark red gums • Bleeding in gums • Bad breath • Tooth loss • Pus in gums Causes: • Neglecting dental hygiene gives rise to bacteria which leads to infection • Incorrect eating habits • Brushing aggressively Natural home remedy using orange or lemon peels: 1. Take some orange or lemon peels 2. Rub on the gums for 5 min 3. Do this 2 times a day Natural home remedy using pomegranate, salt and pepper: 1. Take 2 tsp of crushed pomegranate 2. Add ½ tsp black pepper 3. Add 1 tsp salt 4. Mix well 5. Apply this paste on the gums 6. Massage for 5 min 7. Gargle with lukewarm water If pomegranate is not available, apply mixture of salt and pepper Natural home remedy using spinach and carrot: 1. Take a handful of spinach leaves 2. Add 1 chopped carrot 3. Crush the two and make a paste 4. Press the paste on a sieve and extract its juice 5. Drink this juice 3 times a day Tips: • Eat 1 bowl of chopped cabbage and 1 banana every day. They both have nutrients which help improve gum disease

Wednesday, July 1, 2015

YATAMBUE MAGONJWA YA NGONO UYAEPUKE


Mfumo wa uzazi unaweza kuathiria na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya ngono ambayo hushambulia mfumo huo, leo tutajadili baadhi ya magonjwa hayo ambapo tutapata kujua majina yao, jinsi yanavyoambukizwa, dalili na kinga au tiba zao ijapokuwa kipengele cha tiba sitakiongelea kwa undani.

1. KISONONO:
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi na hushambulia zaidi sehemu za siri za jinsia zote.

Dalili;
Dalili kuu za ugonjwa huu ni mgonjwa kutokwa na usaa kwenye sehemu za siri na mgonjwa kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo, na ukikaa kwa muda mrefu bila kutibiwa huenea zaidi kwenye viungo vingine vya uzazi.

Kuzuia/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni kuacha kujamiiana au kutumia kondom kwa kila tendo la ngono.
na kwa wale ambao tayari wanamaambukizi wanashauriwa kutibiwa wote hospitalini na kuacha kufanya ngono hadi wapone.


2. KASWENDE:
Huu ni ugonjwa wa ngono unaosababishwa na bakteria.

Dalili;
Mgonjwa wa Kaswende hupata mwasho mkali sehemu za siri na kupata vijeraha vidogo vidogo sehemu hizo na akikaa sana na ugonjwa huo bila kutibiwa huweza kuathirika sehemu zingine za mwili kama vile, Moyo, ubongo na hatimaye kusababisha kifo.

Kinga/ Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni; kuacha kujamiiana na ukishindwa kuacha kabisa basi fanya ngono iliyo salama(yaani utumie Condom)

Ugonjwa huu hutibiwa Hospitalini na inashauriwa  wenza wenye ugonjwa huu watibiwe kwa pamoja.
Wakati wa matibabu maswala ya kujamiiana yawekwe kando hadi matibabu yakamilike kwani yanaweza yakaongeza maambukizi mapya.

3. KLAMEDIA:
Huu ni mojawapo ya magonjwa ya ngono ambao haujafahamika unaambukizwa na wadudu wa aina gani.

Dalili;
Mgonjwa wa klamedia hutokwa na uchafu  katika sehemu zake za siri na kupata maumivu makali wakati wa haja ndogo na wakati wa kujamiiana.

Kinga/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni sawa na kinga ya magonjwa mengine ya zinaa, ili usiupate ugonjwa huu unashauriwa kuacha kabisa kufanya ngono au kutumia condom kwa kila tendo la ndoa.

Hugonjwa huu pia hutibiwa hospitalini.

4. TRIKOMONA:
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa (trikomonasi vaginalis) ambazo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Dalili;
Dalili za ugonjwa huu hutofautiana kwa kila jinsia.
WANAWAKE: Wanawake wenye ugonjwa huu hupatwa mwasho mkali  katika sehemu za siri,
                           Hutokwa na uchafu wa rangi ya njano au kijani wenye harufu mbaya sehemu za siri.

WANAUME:    Wanaume wenye ugonjwa huu hupata maumivu makali wakati wa haja ndogo.

Kinga/ Tiba;
Ugonjwa huu pia unazuilika kwa kuacha kujamiiana au kutumia condom kwa kila tendo la ngono.
Mgonjwa atatibiwa hospitalini na kupona kabisa.

CHAKULA WAKATI WA MIMBA

Madaktari wengi wanashauri kunywa madawa ya vitamin sababu wajawazito wengi hawali vizuri. Madini ya muhimu kwa mtoto ni kama yafuatayo; Calcium, Iron, Folate (B vitamin). Haya madini yote yanaweza kupatikana kwenye vyakula vifuatazo; Calcium: Mtoto anahitaji Calcium kwa ajili ya kukuza viungo vya mwili na mifupa kukomaa vizuri. Mwili wako unanyonya Calcium inayohitajika na mtoto hivyo basi unahitaji kula vyakula vitakavyoongeza kiasi hichi mwilini. Lakini pia ili Calcium inyonywe na mwili unahitaji kukaa juani kwa kipindi kama cha dakika kumi kila siku. Calcium hupatikana kwenye, maziwa, mboga za majani kwa wingi, Mayai (Hakikisha yameiva vizuri )Samaki (esp mifupa lakini sio samaki wote wanashauliwa kula wakati wa mimba), maharage ya soya, na mchele. Madini ya Chuma (Iron) Chuma ni muhimu kwa utengenezaji wa damu, kwani kipindi hichi damu nyingi inahitajika kwa ajili ya kumpelekea mtoto chakula. Wajawazito wengi huwa vichanga vyao vinakufa sababu ya ukosefu wa damu toka kwa mama. Iron hupatikana toka kwa vyakula kama; Mboga za majani kwa wingi zaidi (Matembele yana Iron zaidi, mchicha, brocolli, sukuma wiki n.k). Chai na Kahawa huwa inasaidia kuzuia kunyonywa ka iron mwilini hivyo epuka kunya chai nyingi na ikiwezekana uache kunywa kahawa kwa kipindi hiki.

UGONJWA WA KIFAFA KWA WATOTO (seizures)

Kifafa mara nyingi husababishwa na uvujaji wa wave za kama za umeme (electrical discharge) kwenye ubongo ama husababishwa na hali ya kuzimia (baada ya kupunguka kwa msukumo wa damu ubongoni). Dalili (symptoms) zinaweza hutofautiana kulingana na sehemu ipi ya ubongo imehusika, lakini mara nyingi utasikia hali ya mwili kusisimka sio kwa kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe, na pia kupoteza fahamu. Baadhi ya vifafa vingine huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa sukari kwenye damu, maambukizi, kuuumia kichwa(head injuries), ajari za barabarani au kuoverdose madawa ya kulevya. Pia kifafa kinaweza sababishwa na uvimbe kwenye ubongo ama tatizo linguine la afya linaloathiri ubongo. Kifafa mara nyingi hutokea zaidi ya mara moja. Watoto wa chini ya miaka 5 huwa wanapata hali ya kifafa pale joto lao la mwili linapozidi degree 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa inaitwa Febrile seizure. Hii inaogopesha kama mzazi lakini hii hali ni ya dakika chache tuu, mara chache husababisha matatizo makubwa, especially kama joto hili limesababishwa na maambukizi kama meningitis. Kwa watoto chini ya miaka 5, kuhold pumzi inaweza sababisha hali ya kifafa (seizure). Kuna watoto wakati wanapokasirika huwa wanashikiria pumzi (hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tuu ya kuachia kilio kikubwa, kabla ya kupoteza fahamu kifafa kufuatia. Mara nyingi hali hii huisha yenyewe. Watoto wa umri zaidi ya miaka 5 wachache huwa na hali hii lakini mara nyingi huwa inaisha baada ya sekunde chache. Kama mtoto wako ana kifafa ufanyeje Kama mtoto wako amepatwa na kifafa basi unashauriwa kumlaza chini sehemu ambayo ni salama, wanashauri umlaze upande wake wa kulia. Ondoa kitu chochote cha hatari ambacho kipo karibu, kama vyupa, sindano, mawe n.k. Kama ana cheni shongoni ivue ama kama nguo ipo shingoni ivue pia isimkabe. Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake. Mara tuu kifafa kinapoisha basi mfariji mtoto, ni muhimu kwa watoto kubaki kulala chini mpaka hali hii iishe kabisa nay eye mwenyewe akitaka kuinuka. Tafadhari mwite daktari pale ambapo kifafa kinaendelea zaidi ya dakika 5, pia kama mtoto ana vitu vifuatavyo: . anashindwa kupumua .ameumia kichwa .ana magonjwa ya moyo .hajawahi kupata kifafa zamani .kama amekunywa sumu ama ameoverdose dawa. Baada ya kifafa, mtoto huonekana kuchoka, amechanganyikiwa, na anaweza kulala usingizi mzito sana (postictal period) hauhitaji kumwamsha mtoto as long as anapumua vizuri. Usijaribu kump chakula mpaka mtoto aamke na aonekane kuchangamka.

TATIZO LA KUTOKULALA KWA WATOTO WACHANGA

Watoto wengi wadogo huwa wanapata shida sana kutulia na kulala wakati wa usiku. Kwa watu wengine hili sio tatizo kwao na kama haikusumbui mtoto wako kwenda kulala muda ambao wewe unaenda kulala, basi sio shida. Lakini, kama wewe, ama mtoto wako anasumbuka na tatizo la kushindwa kulala usiku unaweza kujaribu kufanya yafuatayo: Kila mtoto ni tofauti na fanya tuu kile unachoona kinafaa kwa mwanao. Kama Mtoto wako hataki kwenda kitandani: Amua saa ngapi ama mda gani unataka mtoto awe anaenda kitandani. Kwa kuanza, mda wa mtoto kwenda kulala ukikaribia (ule mda anaolalaga kila siku) anza kumpeleka kulala dakika 20 kabla kwa siku ya kwanza, alafu siku ya pili mpeleke dakika 30 kabla, ya tatu iwe dakika 40 kabla na kuendelea kuongeza dakika 10 kila siku mpaka ifikie mda ule unaotaka wewe. Jipangie kikomo cha kukaaa na mwanao kitandani wakati wa kulala, mfano msomee hadithi moja tuu, alafu sema usiku mwema, muage na kumwacha alale. Mpatie mtoto wako toy yake anayoipenda alale nayo, mfano kama huwa anatumia dummy ya mdomoni, ama kitaulo (kuna watoto hunyonya kitaulo) ama chochote kitakachombembeleza kulala. Kama mtoto wako analia, umwache kitandani na uondoke chumbani na mpatie dakika 5 mpaka 10 ya kujituliza mwenyewe kabla ya kumyamazisha tena. Usimnyanyue ama kumbeba mtoto, ama kumtoa kitandani na kama mtoto atainuka na kutoka kitandani basi mchukue na kumrudisha kitandani tena. Washa taa yenye mwanga mdogo (kama unayo) ama acha mwanga wa mbalamwezi uingie kama kutakuwa na ulazima huo. Hakikisha amelala kabla ya kwenda kumwangalia mtoto ili usimwamshe tena. Fanya hivi kila siku na usikate tamaa baada ya siku moja tuu, jipatie siku 5 ili mtoto awe na mazoea. Kama mtoto anaamka mara kwa mara usiku. Ni kawaida kwa watoto wa zaidi ya miezi 6 kulala usiku mzima bila kuamka, Hata hivy, kuna watoto wengi chini ya miaka mitano huwa hawalali usiku mzima bila kuamka. Kuna ambao watarudi kulala tena wao wenyewe na wengine ambao watalia kwa kutaka uwepo wa mtu. Kama hii hali itatokea, jaribu kutatua tatizo linalimfanya mwanao aamke usiku. Je ni njaa? kama mwanao ni mkubwa zaidi ya mwaka moja, maziwa na uji huwa yanaweza mfanya alale usiku mzima kama hivyo ndio alikunywa mda tuu kabla ya kulala. Je ni uoga/hofu ya giza? unaweza kutumia taa za usiku ama unaweza acha taa ya corrido iwake usiku. Je ni ndoto mbaya? kama ni hivyo jaribu kutafuta kama kuna kitu kinachowasumbua ambacho ndio husababisha kuota usiku. Je ni joto/ baridi kali? kama ni hivyo punguza ama uongeze nguo za kujifunika ama punguza/ongeza joto ama baridi kwenye chumba kwa kufungua milango ama kupunguza AC. Kama hakuna sababu maalumu inayomfanya mwanao aamke, alie ama kutaka ukae nae usiku basi jaribu yafuatayo: Mda wa kuamka - kama mwanao huamka wakati huo huo kila usiku basi jaribu kumwamsha kati ya dakika 15 mpaka 60 kabla alafu mbembeleze tena kurudi kulala. Mruhusu mtoto alale chumba kimoja na kaka yake ama dada yake kama tatizo ni kuogopa kuwa peke yake. Hii itawasaidia wote walale usiku mzima. Mfundishe mwanao kujirudisha kulala yeye mwenyewe usiku, kwanza kama kila kitu kiko sawa, mmbembeleze mwanao kulala bila ya kuongea nae sana akiwa kitandani. Kama anataka kinywaji mpe maji ila angalisho usimpatie chakula wakati akiwa ameshtushwa na usingizi. Ili njia hii ifanye kazi ni lazima umwache mtoto kitandani na usimnyanyue na kwenda nae sebuleni, ama chumbani kwako. Mwache alie kwa kati ya dakika 5 hadi 10 ndipo ukamwangalie tena. Mwambie arudi kulala na mwakikishie kwamba hakuna kitu cha kuogopesha na usiongee nae kitu kingine, kama ni mtoto mchanga mbembeleze kwa kumpapasa mgongoni akiendelea kulia mbebe kwa dakika 2 tuu alafu mrudishe kitandani. mwache kama analia ikifika dakika 10 nenda tena, fanya kama hapo juu na umwache ena ajirudishe kulala. Endelea hivyo kwa siku kadhaa na mtoto atazoea na kuanza kusinzia mwenyewe ukimweka kitandani. Msaidiane na mumeo, mnaweza mkafanya zamu ya kumwangalia mtoto anapolia, hii pia husaidi mtoto kuwajua na kuwazoea wazazi wote wawili, pia itamfanya mama asichoke sana. Ndoto za kutisha Ndoto za kutisha ni kawaida kabisa. Wao mara nyingi huanza kati ya umri wa miezi 18 na miaka mitatu. Ndoto hizi ni si kawaida ni ishara ya masumbuko ya hisia. Huwa inaweza kutokea kama mtoto wako ana wasiwasi juu ya kitu au amepata hofu na kipindi ama hadithi aliyoangalia kwenye luninga. Baada ya ndoto, mtoto wako atahitaji faraja na uhakika. Kama mtoto wako anaota ndoto hizi sana na hujui ni kwa nini basi ongea na daktari. Kuweweseka usiku Hutokea kabla ya umri wa mwaka moja ingawa pia ni kawaida zaidi kwa watoto kati ya umri wa miaka mitatu hadi nane. mara nyingi mtoto huweweseka na kupiga kelele ama kupigapiga mikono na miguu akiwa bado yupo usingizini. hutokea baada masaa machache ya kulala, wanaweza kukaa na kuongeaongea wakiwa usingizini na kuonekana wenye hofu wakiwa usingizini. Wala usiogope na mtoto wako itafika wakati itapita tuu. Usimwamshe mwanao wakati akiweweseka ila kama hutokea mda huohuo kila usiku basi jaribu kumwamsha dakika 15 kabla ya muda ule anaoweweseka kila siku. abaki macho kwa dakika chache kabla ya kumrudisha kulala tena.

FUNGUS WAKATI WA MIMBA (thrush)

Ni kawaida kabisa kutokwa na majimaji mazito (vaginal discharge) ukeni wakati ukiwa na ujazito. Usiwe na wasiwasi kama majimaji haya ni myepesi na yana muonekano wa rangi ya maziwa. Dalili za kuwa na fungus ukeni: · Majimaji yakiwa mazito, myeupe na rangi ya maziwa, na yanayoonekana kama cottage cheese, ama maziwa ya mgando, ama yaliyoharibika. · Kama unawashwa, na kusikia kuvimba kama vile umejikwaruza, na muonekano wa uwekundu sehemu ya ukeni. · Inauma wakati wa kujamiiana · Unasikia kuchomwachomwa wakati unakojoa Je nilipataje thrush: Maambukizi ya ukeni wakati wa mimba ni ya kawaida. Thrush husababishwa na fungus (yeast) wanaoitwa candida albicans ambao wapo na huishi kwenye miili yetu bila kusababisha tatizo lolote. Wapo pia kwenye mfumo wa chakula na mara nyingi hawana madhara yoyote kwetu na wala hautojua kama wapo. Huwa wanaleta tatizo pale tuu wakati fungus hawa na vijidudu vingine ndani na nje ya mwili vinapopungua ama kuongezeka kuliko kiasi kinachitakiwa. Unaweza kupata thrush pale ambapo: · Unapokuwa mjamzito mabadiliko ya hormones kwenye mwili husababisha mwili uwe na sukari nyingi kuliko kiasi inayoitwa glycogen ambayo husababisha fungus kuzaliana kwa wingi (wanatumia glycogen kama chakula na hivyo kuwapatia nguvu ya kujiongeza idadi). · Unapotumia antibiotics, dawa hizi huua vijidudu mwilini ambapo pia huua vijidudu vizuri vinavyopigana na vile vibaya, hivyo basi balance ya vijidudu hivi inakuwa imebadilika na hiyo kusabaisha vile vibaya vizaliane kwa nguvu. · Kisukari (Diabetes): kama una ugonjwa wa kisukari ambacho huujakicontrol pia husababisha thrush. · Kama immune system yako ni dhoofu. Hii inaweza kutokana na pia na matibabu ya magonjwa kama sarakani (cancer) ama magojwa na HIV. Ingawa thrush sio magonjwa ya zinaa, yanawezekana kuambukizwa kama partner wako amepata maambukizi haya, hivyo mnashauriwa wote wawili mpate matibabu kwa wakati moja. Kama unafikiria una thrush, tafadhari mwone daktari. Daktari atakupatia dawa, ingawa wanashauri kutotumia chochote kipindi cha mlongo wa kwanza wa mimba (miezi 3 ya mwanzo) . Dawa zingine ni za kuweka ukeni (kidonge), unashauriwa kuweka usiku wakati umelala ili inyonywe vizuri wakati umelala. Thrush ni vigumu kupona upesi hivyo basi ni vyema umalize dozi utakayopewa na daktari. Tafadhari usichukue dawa za vidonge ambayo utahitaji kumeza, bado haijajulikana kama vina madhara gani kwa mtoto. Je nifanyeje · Wakati unapojiosha ukeni, usitumie sabuni osha na maji masafi (sio ya kisima) ikiwezekana jichemshia maji kidogo tuu(kuua vijidudu) kwa ajili ukeni. Na ikiwezekana jioshe mara moja kwa siku kwani kujisafisha sana ukeni unaondoa wale wadudu wanaohitajika kulinda uke (Good Flora microorganism). · Usitumie mafuta yatakayoirritate ngozi kama pedi za kunukia, deodorant za ukeni, na sabuni zakunukia. · Kula maziwa mgando yasiyo na sukari, ama ingiza maziwa ya mgando ukeni. · Kama utatumia maziwa mgando, njia rahisi ya kuweka ukeni ni kwa kutumia tampoo, chovya tampoo kwenye maziwa mgando, dumbukiza tampoo ukeni, iache kwa muda wa lisaa limoja, alafu itoe. · Kupunguza kueneza thrush, basi jifute toka mbele kwenda nyuma kila baada ya kutumia choo. · Vaa chupi za cotton 100% · Wakati wa kujamiiana tumia kilainisho(lubricant) kupunguza maumivu kama una thrush. Je thrush itamfikia mtoto tumboni Hapana, mtoto amefunikwa na mfuko na hatadhurika. Hata hivyo ni muhimu kupata matibabu kabla ya kujifungua, kwani mtoto anaweza kuambukizwa wakati akitokea ukeni. Kama hii ikitokea basi utahitaji matibabu wewe na mtoto, mtoto mara nyingi anakuwa na utando mweupe kwenye ulimi. Utagundua thrush huja na kuondoka wakati wa mimba, na huchukua mda mrefu kuitibu lakini sio kitu cha kuogopa sana.

KUTAPIKA NA KUHARISHA KWA MTOTO

Ni kawaida kwa watoto wachanga na watoto kutapika. Katika kesi nyingi , kutapika hudumu kati ya siku moja mpaka mbili na si ishara ya kitu chochote kikubwa . Kawaida sababu ya kutapika kwa watoto ni gastroenteritis . Haya ni maambukizi ya kolomeo kawaida husababishwa na virusi au bakteria. Na pia husababisha kuhara . Mfumo wa kinga ya mtoto wako kwa kawaida hupigana na maambukizi baada ya siku chache. Watoto mara nyingi pia hutapika wakati wanapomeza hewa wakati wa kulishwa . Hata hivyo , kuendelea kutapika wakati mwingine inaweza kuwa ni ishara ya kitu kibaya zaidi , ikiwa ni pamoja maambukizi makali kama vile uti wa mgongo. Ukurasa huu unaeleza nini cha kufanya kama mtoto wako anaendelea kutapika na iuaelezea baadhi ya sababu ya kawaida ya kutapika kwa watoto wachanga, na watoto kwa ujumla . Kama mtoto wako ana joto la juu , unaweza pia kusoma kuhusu homa kwa watoto Nini cha kufanya. Kama mtoto wako anatapika, unapaswa kufuatilia hali kwa uangalifu mkubwa. Amini moyo wako na mpeleke kwa dakitari wako mara moja kama wewe una wasiwasi. Kama sababu ni tummy bug tuu (kuhara kwa kawaida kwa mtoto ama tummy flu), atakula na kucheza kama kawaida. Katika kesi hiyo, endelea kumlisha kama kawaida na kumpatia kinywaji (maji, juice n.k) mara kwa mara. Maji humsaidia kutopunguka kwa uwingi wa maji mwilini ambao ni hatari. Lakini kama haonekani wa kawaida, - kwa mfano, kama yupo floppy , hasira , kutojibu, au amepoteza hamu ya kula - inawezekana anaumwa, hivyo unapaswa kuwasiliana na daktari wako mara moja. Kumpeleka kwa daktari Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kama : •Mtoto wako amekuwa akitapika kwa zaidi ya masaa 24 • Mtoto wako anatapika ndani ya masaa nane, au kama unafikiri amepungukiwa na maji mwilini. • Kama ni floppy, mwnye hasira, anagoma chakula , au hayupo kwenye hali ya kawaida , • Ana maumivu makali tummy • Ana maumivu ya kichwa na shingo ngumu. Ishara ya upungufu wa maji mwilini Kutapika kali na kuhara kunaweza kwa urahisi kusababisha upungufu wa maji mwilini , hasa katika watoto wachanga. Hii ina maana mwili wa mtoto wako hana maji ya kutosha mwilini au hana chumvi inayohitajika kwa ajili ya mwili kufanya kazi kwa kawaida . Watoto wenye upungufu wa maji mara nyingi hujisikia na huonekana kuumwa. Ishara ya upungufu wa maji mwilini ni : • kinywa kikavu • kilio bila kutoa machozi • kukojoa kidogo sana au kiasi cha nappies anazokojolea kupunguka. • Kuongezeka kwa kiu • Kudhoofika Ufanyaje Jambo muhimu zaidi unaweza kufanya kama mtoto wako anatapika ni kuhakikisha anaendelea kunywa maji ya kunywa. Kama mtoto wako anatapika , endelea kumnyonyesha. Kama wamepungukiwa maji, , atakuwa anahitaji maji ya ziada. Uliza mfamasia wako kama wangeweza kupendekeza kumpatia dawa ya kusaidia kutopunguka kwa maji mwilini. Dawa hii ni poda maalum unaitengeneza kwa kuweka kwenye maji. Ina sukari na chumvi katika kiasi maalum ya kusaidia kuchukua nafasi ya maji na chumvi kupotea kwa njia ya kutapika na kuhara. Watoto ambao hutapika wanapaswa kunywa maji haya kidogokidogo hivyo hawatapungukiwa maji mwilini. .Pia motto anaweza kunywa maji , maji mengi kwenye juice ya kuchanganya na maji , diluted maji ya matunda au maziwa. Hata hivyo, kama pia wanaharisha, maji ya matunda ziepukwe. Tena, GP wako au mfamasia anaweza kupendekeza ORS. Dawa ya kusaidia wakati wa kuharisha kwa motto. Sababu ya kutapika kwa watoto. Kuna sababu ya uwezekano wa kutapika katika watoto, ambayo ni ilivyoelezwa hapo chini gastroenteritis Gastroenteritis ni maambukizi ya utumbo. Ni kitu cha kawaida inayosababisha kutapika kwa watoto na kwa kawaida huchukua muda wa siku chache . maambukizo ya hatari Watoto wadogo hasawapo katika hatari ya kupatwa na maambukizi kama vile pneumonia au maambukizi ya figo. Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kama motto ana dalili ya magonjwa haya. ugonjwa wa kidole tumbo Ugonjwa wa kidole tumbo

Friday, June 26, 2015

RAHA!!!!!! JUA VYAKULA VINAVYOREFUSHA UUME>




If you want to increase the size of your penis, you are undoubtedly doing penis enlargement exercises. However, to get the most benefit from your workouts, you need to make sure that your body is well-nourished. Eating the right foods will help with increasing penis size, improving your sexual performance, and even improving the health of your penis and prostate. Seven foods in particular will help you get faster and better results from your penis enlargement program. Here we go 
ALSO READ:8 FOODS THAT INCREASE 5EXUAL STAMINA
1) Cayenne Pepper
If you consume cayenne pepper (the seasoning or the pepper itself) each day, you can strengthen your blood vessels and boost your metabolism.
ALSO READ:8 FOODS THAT INCREASE 5EXUAL STAMINA
2) Dark Chocolate
A small amount of dark chocolate daily can do a lot for your body, including helping your penis grow bigger. Dark chocolate helps you increase your size since it contains flavonoids, which improve circulation.

ZITAMBUE SIRI NA FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU







Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu. 


Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.


Faida za vitunguu swaumu


Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na

  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.


Ushahidi wa Kitafiti 

Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.



Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Nini Madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.